TANZANIA-MAGUFULI-MAAFA-KIVUKO

Miili 209 yaopolewa katika ajali ya kivuko nchini Tanzania

Juhudi za kunasua miili zinaendelea Ziwani Victoria, nchini Tanzania kufuatia kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere
Juhudi za kunasua miili zinaendelea Ziwani Victoria, nchini Tanzania kufuatia kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere http://www.mwananchi.co.tz/

Ripoti kutoka Tanzania zinasema kufikia sasa idadi ya miili 209 ya watu waliopoteza maisha kufuatia kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere kilichokuwa kikifanya safari katika Ziwa Victoria imefikia 209. 

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Tanzania, Mhandisi Isack Kamwelwe amearifu hayo, akizungumza na wanahabari Wilayani Ukerewe mkoani Mwanza wakati akitokea takwimu za karibuni.

"Miili 209 imeopolewa na tayari 172 imetambuliwa na kuchukuliwa na ndugu zao na waliokolewa wakiwa hai wamefikia 41,"amesema Waziri Kamwelwe, akizungumza katika tukio lililorushwa na kituo cha utangazaji cha Taifa.

Waziri huyo pia ameeleza kwamba juhudi za uokozi zitaendelea.

Katika hatua nyingine serikali ya Tanzania imeanza kupokea rambirambi kutoka kwa watu mbalimbali kufuatia msiba huo mzito ulioitikisa Tanzania.

Mwandishi wa Habari Martin Nyoni akiwa katika kisiwa cha Ukara, kulikotea ajali hiyo Jumamosi asubuhi ameripoti kuwa, mili zaidi ilipatikana asubuhi na idadi kufika zaidi ya watu walipoteza maisha kuwa zaidi ya 140.

Juhudi za kutafuta miili zaidi inaendelea na inatarajiwa kumalizika siku ya Jumapili huku idadi ya watu waliopoteza maisha ikitarajiwa kuongezeka.

Usikose kusikiliza matangazo yetu saa 12 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki na saa 11 kwa saa ya Afrika ya Kati.