KENYA-USALAMA

Ishirini na moja wajeruhiwa katika makabiliano Narok, Kenya

Vikosi vya usalama nchini Kenya vyatumwa katika eneo la tukio.
Vikosi vya usalama nchini Kenya vyatumwa katika eneo la tukio. Reuters

Watu 21 wamejeruhiwa baada ya kuzuka tena kwa mapigano kati ya jamii mbili zinazoishi katika Kaunti ya Narok nchini Kenya. Polisi inasema inaendelea kuwasaka wahusika.

Matangazo ya kibiashara

Mwakilishi wa serikali katika eneo hilo George Natembeya amesema, mapigano hayo yalizuka siku ya Jumapili baada ya familia moja kuibiwa mifugo yake.

Waliojeruhiwa walichomwa na mishale, na wamepelekwa hospitali kupata matibabu.

Waathirika wanne wamekubaliwa kwenye Hospitali ya Tenwek Mission huko Bomet County.

Maofisa wa usalama wamepelekwa eneo hulo baada ya tukio hilo.

Makabiliano kati ya jamii hizo mbili huwa mara kwa mara ikitokea, lakini haijajulikana chanzo cha migogoro kati ya jamii hizo.