UGANDA-AFYA-EBOLA

Uganda: Tumeweka mikakati ya kuzuia maambukizi ya Ebola

Maafisa wa afya wakibeba mwili wa mgonjwa wa Ebola ambao hajathibitishwa huko Mangina, karibu na Beni, mkoa wa Kivu Kaskazini, Agosti 22, 2018.
Maafisa wa afya wakibeba mwili wa mgonjwa wa Ebola ambao hajathibitishwa huko Mangina, karibu na Beni, mkoa wa Kivu Kaskazini, Agosti 22, 2018. © AFP

Uganda inasema hakuna uwezekano wa maambukizi ya ugonjwa hatari wa Ebola ambao umewaathiri wakaazi wa Beni Mashariki mwa DRC, kufika nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Hivi karibuni mgonjwa mmoja, katika mpaka wa nchi hizo mbili, kutoka kijiji cha Kasenyi alipata matibabu katika hospitali ya Uganda na baadaye kupoteza maisha, baada ya kushukiwa alikuwa anasumbiliwa na ugonjwa wa Ebola.

Wizara ya afya nchini humo inasema imeweka mikakati kuhakikisha kuwa inazuia maambukizi ya Ebola kufika nchini humo.

Wilaya ya Beni mashariki mwa DRC iliyokumbwa na mlipuko huu wa ugonjwa hatari wa Ebola inapakana na Uganda, na watu kutoka wilaya hiyo na maeneo jirani ya Uganda wamekuwa wakitembeleana bila wasiwasi.

Watu kutoka maeneo hayo ya Uganda wamekuwa na hofu ya kuambukizwa virusi vya Ebola, kutokana na kuwa na ukaribu na watu kutoka Beni, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.