KENYA-HAKI

Gavana wa kaunti ya Migori Obado aendelea kuzuiwa jela

Mji mkuu wa Kenya, Nairobi.
Mji mkuu wa Kenya, Nairobi. Yasuyoshi CHIBA / AFP

Gavana wa kaunti ya Migori Okoth Obado ataendelea kuzuiwa rumande kwa siku 12 zaidi, baada ya Mahakama kumyima dhamana, umuzi ambao umekosolewa na watu wa familia ya mshtumiwa pamoja na mawakili wake.

Matangazo ya kibiashara

Wanasheria wa Obado walipinga uamuzi huo wakidai kuwa hakuna ithibati kwamba anaweza kutatiza uchunguzi kwani amekuwa akishirikiana na wachunguzi tangu walipoanza shughuli hiyo. Aidha walisema kwamba kulingana na katiba kila mshukiwa ana haki ya kuachiliwa kwa dhamana.

Obado anakabiliwa na mashataka ya kumuua Sharon Otieno, mwanafunzi wa chuo kikuu aliyekuwa na uja uzito wake wa miezi saba.

Uchunguzi ulibaini kuwa mwanafunzi huyo alibakwa na kisa kuchomwa kisu mara nane na mwili wake kutupwa msituni.

Gavana huyo amekanusha shutma hizo dhidi yake.

Obado amekuwa akizuiliwa rumande tangu alipotiwa mbaroni Ijumaa wiki iliyopita. Akitoa uamuzi wa kuendelea kuzuiliwa kwa Gavana Obado Jaji Jessie Lessit Jumanne alisema ulikuwapo uwezekano wa kuwatishia mashahidi.

Vile vile imebainika kuwa wachunguzi wanawalenga watu fulani walio na uhusiano wa karibu na Obado ili kufanikisha uchunguzi wao.