Pata taarifa kuu
EAC-BURUNDI-SUDAN-KUSINI-SIASA-USALAMA

EAC yaombwa kutafutia ufumbuzi mgogoro wa kisiasa nchini Burundi na Sudan Kusini

Marais wa Nchi za Afrika Mashariki katika mkutano wa mwisho Dar es Salaam tarehe 31 Mei.
Marais wa Nchi za Afrika Mashariki katika mkutano wa mwisho Dar es Salaam tarehe 31 Mei. AFP PHOTO / STRINGER
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Wabunge nchini Uganda wanaoketi katika Kamati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, wanaitaka Jumuiya hiyo kufanya zaidi kuhusu hali ya kisiasa nchini Burundi na hali ya usalama nchini Sudan Kusini.

Matangazo ya kibiashara

Wakizungimza katika Makao Makuu ya Jumuiya hiyo, mjini Arusha nchini Tanzania, baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na spika wa bunge la Jumuiya hiyo, Martin Ngoga, wamesema kuna umuhimu suala la Burundi kupatiwa ufumbuzi haraka iwezekanavyo.

Spika Ngoga amesema, pamoja na juhudi zinazofanywa katika maendeleo ya Jumuiya hiyo, kuna umuhimu wa kuwa na mazungumzo ya wazi kuhusu utekelezwaji wa mikataba mbalimbali katika jumuiya hiyo.

Aidha, ameshangazwa na mzozo wa Sudan Kusini kuachiwa nchi za IGAD, badala ya Jumuiya hiyo kushughulikia suala hili.

Nchi hizi mbili, wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zinaendelea kukumbwa na mgogoro wa kisiasa na hali hiyo imesababisa jumuiya hiyo kuendelea kunyooshewa kidole cha lawama kwamba inaegemea upande fulani.

Machafuko katika nchi hizo mbili yamesababisha vifo vya raia wengi na maelfu wengine kuyatoroka makaazi yao, huku wengi wakikimbilia katika nchi jirani, wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, na hilo limekua ni mzigo mkubwa kwa nchi hizo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.