Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-AFRIKA KUSINI-USALAMA

Afrika Kusini yaendelea na jitihada za kupatikana kwa amani Sudani Kusini

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir (kushoto), hasimu wake Riek Machar (kulia) na Rais wa Sudan Omar al-Bashir wakati wa sherehe ya kutia saini kwenye "Azimio la Khartoum" huko Khartoum tarehe 27 Juni 2018.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir (kushoto), hasimu wake Riek Machar (kulia) na Rais wa Sudan Omar al-Bashir wakati wa sherehe ya kutia saini kwenye "Azimio la Khartoum" huko Khartoum tarehe 27 Juni 2018. REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Makamu rais wa Afrika Kusini David Mabuza yupo jijini Khartoum nchini Sudan kushinikiza utekelezaji kikamilifu kwa mkataba wa amani nchini Sudan Kusini.

Matangazo ya kibiashara

Mjumbe huyo wa serikali ya Afrika Kusini anakutana na viongozi wa Afrika Mashariki, marais wa Kenya na Uganda kujadiliana nao kuhusu namna mkataba huo uliotiwa saini mwezi Septemba unavyoweza kuanza kutekelezwa kati ya serikali ya Juba na waasi.

Mwaka 2013 viliibuka vita vya wenyewe kwa wenye vikivipambaisha vikosi tiifu kwa rais Salva Kiir, na vile vinavyomtii makamu wa zamani wa rais Riek Machar.

Mnamo mwezi Septemba viongozi wa Sudan Kusini, rais Salva Kiir na kiongozi wa upinzani Riek Machar, kwa mara nyingine walisaini makubaliano ya mwisho ya amani ya kudumu nchini humo, yanayolenga kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimedumu kwa miaka mitano na kusababisha vifo vya maelfu ya watu. Machar sasa atakuwa makamu wa kwanza wa rais katika serikali ya mpito itakayoundwa.

Sudan Kusini inapakana na Sudan, Kenya, Ethiopia, Uganda na DRC.

Sudan Kusini ndiyo nchi changa kabisa duniani. Ilipata uhuru wake kutoka Sudan mnamo mwaka 2011. Ni nchi yenye utajiri wa mafuta baada ya kuondoka na karibu theluthi mbili ya mafuta ya Sudan.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.