SUDANI KUSINI-MACHAR-SIASA-USALAMA

Wafungwa waliohukumiwa kifo waachiliwa huru Sudan Kusini

Salva Kiir (kulia) na Riek Machar (katikati) Juba Oktoba 31, 2018.
Salva Kiir (kulia) na Riek Machar (katikati) Juba Oktoba 31, 2018. REUTERS/Jok Solomun

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir, ameagiza kuachiliwa huru kwa wafungwa wawili wa kisiasa, msemaji wa zamani wa kiongozi wa waasi Riek Machar na raia mmoja wa Afrika Kusini.

Matangazo ya kibiashara

Kiir alitangaza uamuzi huo hapo jsiku ya Jumatano, wakati wa kushereheka kupatikana kwa mkataba wa amani jijini Juba.

Wafungwa hao wawili, James Gatdet, na William Endley, wanatarajiwa kuwa huru leo Alhamisi, baada ya hapo awali kuhukumiwa kifo.

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir, amesema vita vimemalizika nchini humo na sasa kazi inayosalia ni kuliunganisha upya taifa hilo changa na kuhubiri maridhiano.Sudan Kusini ilipata uhuru wake mwaka 2011.

Akizungumza katika sherehe hizo, baada ya kurejea jijini Juba kwa mara ya kwanza baada ya miaka miwili, Riek Machar ambaye atarejea katika nafasi yake ya kuwa Makamu wa kwanza wa rais, amesema, ana nia ya dhati ya kuhakikisha kuwa mkataba huo unatekelezwa.