MAREKANI-TANZANIA-USHOGA

Marekani yaonya raia wake waishio Tanzania kufuatia hatua dhidi ya mashoga

Kamanda wa Polisi mkoa wa Dar es Salaam nchini Tanzania.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Dar es Salaam nchini Tanzania. Issa Michuzi

Marekani imewaonya raia wake wanaoishi nchini Tanzania, kujihadhari baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kutangaza operesheni ya kuwatafuta na kuwashtaki watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Matangazo ya kibiashara

Katika ujumbe ulioadikwa katika Ubalozi wa nchi hiyo, raia wa Marekani wameshauriwa kupitia upya mitandao ya kijamii na kuondoa chochote kinachoweza kusababishia matatizo.

Wakati huo huo Shirika la kimataifa la Haki za Binadaamu la Amnesty International limelelezea wasiwasi wake kufuatia hatua ya Gavana wa mkowa wa Dar es Salaam Paul Makonda ya kuwataka wakazi wa mkoa huo kuwafichua watu wa mapenzi ya jinia moja (mashoga).

Amnesty International inasema kuwa hatua ya kuwakamata na kuwashikilia watu kutoka jamii hiyo inaendeshwa kwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.

Hata hivyo Wizara ya Mambo ya nje ya Tanzania kupitia taarifa kwa vyombo vya Habari imesema, hatua iliyochukuliwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ni mtazamo wake binafsi na sio msimamo wa serikali.