TANZANIA-AMNESTY-HAKI-USHOGA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam awataka raia kuwafichua mashoga

Jamii ya wapenzi wa jinsia moja waendelea kutengwa katika nchi mbalimbali barani Afrika., Mfano nchini Cameroon ushoga waadhibiwa.
Jamii ya wapenzi wa jinsia moja waendelea kutengwa katika nchi mbalimbali barani Afrika., Mfano nchini Cameroon ushoga waadhibiwa. Getty Images / WOJTEK RADWANSKI

Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda ametoa wito kwa wakazi wa mji huo "kuwataja wapenzi wa jinsia moja na kuwafikisha mbele ya vyombo vya usalama".

Matangazo ya kibiashara

Katika miaka ya hivi karibuni, operesheni ya kamata kamata dhidi ya jamii ya wapenzi wa jinsi moja imekuwa ikiendelea nchini Tanzania. Makonda, mshirika wa karibu wa Rais John Magufuli, na mwenye imani ya Kikristo, amewataka wananchi wenzake kuunga mkono kampeni yake dhidi ya ushoga, ambao, amesema, "umepoteza maadili ya Watanzania na dini zetu zote mbili Ukristo na Uislamu."

Wapenzi wa jinsia moja nchini Tanzania wameendelea kuishi kwa hofu, huku baadhi yao wakilazimika kuishi kwa kujificha.

Wito huu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul makonda umewatia hofu wapenzi wa jinsi moja nchi Tanzania. Kwa mujibu wa shirika la kimataifa la Haki za Binadamu Amnesty International, majina ya watu 5,000 tayari yamefikishwa kwa polisi. Na kwenye mitandao ya kijamii, video zimeanza kusambazwa zikionyesha watu waliokamatwa kwa kusingiziwa tu au kushukiwa. John, mwenye umri wa miaka 25, amekubali kuweka wazi mambo yake, huku akiwa na wasiwasi ... "Hivi sasa, ninaishi na rafiki yangu, katika nyumba moja. Hatujui kama majirani zetu wanatushuku au la ... Lakini wakati mwingine tunaondoka mapema asubuhi na kurejea nyumbani usiku wa manane, yaani kukataa wasituone. "

Si mara ya kwanza Tanzania kuchukuwa hatua kama hizo dhidi ya jamii ya wapenzi wa jinsi moja. Mwaka jana, serikali ilipiga marufuku kuwanunulia wapenzi wa jinsia moja vifaa vinavyowazuia kuambukizwa Ukimwi huku mashirika yasiyo ya kiserikali yakipigwa marufuku kusaidia wagonjwa wa Ukimwi kutoka jamii hiyo.

Septemba 2017, huko Zanzibar, wasichana kumi na mbili na wavulana 8 ambao walikuwa wakifuata semina kuhusu VVU, walikamatwa, baada ya kushtumiwa kuwa ni watu kutoka jamii ya wapenzi wa jinsi moja ushoga.

"Tunaogopa! Mwaka jana, mmoja wa marafiki zangu alikamatwa na walipomkamata, walimbaka ... kabla ya kupelekwa jela. Sio vizuri kabisa. Tunasumbuliwa hapa na hatujui nani anayeweza kutusaidia. "

Taasisi za kimataifa na wanadiplomasia nchini Tanzania wamesalia kimya. Kwa upande wake, serikali ya Tanzania imejitokeza na kuwa ya kwanza kulaani hatua hiyo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na kuhakikisha kuwa Tanzania inaheshimu mikataba yote ya kimataifa kuhusu haki za binadamu ambazo ilitia saini.