TANZANIA-EU-HAKI ZA BINADAMU

Uhusiano kati ya Umoja wa Ulaya na Tanzania waingia dosari

Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Balozi Roeland van de Geer, akiwa na Rais wa Tanzania, John Magufuli
Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Balozi Roeland van de Geer, akiwa na Rais wa Tanzania, John Magufuli Ikulu/Tanzania

Umoja wa Ulaya umesema utaangalia upya uhusiano wake na Tanzania. Hayo ni baada ya mwishoni mwa juma lililopita umoja huo kumuita nyumbani mwakilishi wake nchini Tanzania, Balozi Roeland van de Geer.

Matangazo ya kibiashara

Wakti huo Umoja wa Ulaya ulisema umemuita mjumbe wake nchini Tanzania kwa mashauriano pamoja na kutathmini upya uhusiano wake na nchi hiyo kutokana na kuongezeka kwa ukiukaji wa haki za binaadamu Tanzania.

Kupitia taarifa iliyotolewa mapema wiki hii, Umoja wa Ulaya unasema unasikitishwa na kushuka kwa haki za binadamu nchini humo.

Uamuzi wa Umoja wa Mataifa ulikuja siku chache baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kuwataka wananchi kuwafichua watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja na kuwafikisha mkononi mwa vyomvo vya usalama.

Hata hivyo hatua hiyo ya Makonda ulitupiliwa mbali na serikali ya Tanzania ikibani kwamba Tanzania ni nchi ambayo inaheshimu haki za binadamu, baada ya kuweka saini kwenye mikataba mbalimbali ya kimataifa kuhusu haki za binadamu.

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya nje ya Tanzania iliyotolewa Jumapili, Novemba 4 inadai kampeni hiyo ni mawazo binafsi ya Makonda na si msimamo rasmi wa serikali.

Mapenzi ya jinsia moja ni haramu katika baadhi ya nchi Afrika ikiwemo Tanzania.