TANZANIA-CANADA-DIPLOMASIA

Balozi wa Tanzania nchini Canada aondolewa kazini na kuvuliwa hadhi ya ubalozi

Alphayo Kidata aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada
Alphayo Kidata aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada Mwananchi

Rais wa Tanzania, John Magufuli amemfukuza kazi Balozi wa Tanzania nchini Canada, Alphayo Kidata.

Matangazo ya kibiashara

Taarifa iliyotolewa jana na Wizara ya Mambo ya Nje ilisema utenguzi wa kiongozi huyo umekwenda sambamba na kuvuliwa hadhi ya ubalozi.

Kidata ni miongoni mwa waofisa waandamizi walioshika nafasi nyeti katika serikali ya Tanzania tangu mwaka 2015.

Awali Rais Magufuli alimteua kuwa Kaimu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato, akichukua pahala pa Rished Bade aliyefutwa kazi, kisha alithibitishwa rasmi kuwa Kamishna wa mamlaka hiyo yenye wajibu wa kukusanya kodi nchini Tanzania.

Hata hivyo, Kidata hakudumu kwenye nafasi hiyo ambapo baadaye kidogo aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu Ikulu, akichukua nafasi ya Peter Ilomo aliyestaafu kwa mujibu wa sheria.

Hata hivyom Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania katika tamko lake haikueleza kinagaubaga chanzo cha kufutwa kazi kwa Kidata na kuondolewa hadhi ya ubalozi.

Kwa mujibu wa katiba ya Tanzania, Rais ana mamlaka ya kuteuwa maofisa mbalimbali wa serikali ya Tanzania wakiwemo mabalozi.