TANZANIA-KATIBA-JOHN MAGUFULI

Joseph Butiku: Watanzania bado wanahitaji katiba mpya

Mwanasiasa Mkongwe nchini Tanzania, Joseph Butiku
Mwanasiasa Mkongwe nchini Tanzania, Joseph Butiku Azania Post

Mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania, Joseph Butiku amesema mjadala wa kupata katiba mpya ya Tanzania haujafa kwa sababu wenye katiba ni wananchi wenyewe.

Matangazo ya kibiashara

Butiku amekuwa mstari wa mbele kupigia chapuo uwepo wa katiba mpya ya Tanzania badala ya ile inayotumika sasa ambayo ilitungwa mwaka 1977.

Butiku ambaye ni mkurugeniz mtendaji wa mfuko wa mwalimu Nyerere, ametoa matamshi hayo leo wakati wa maadhimisho ya miaka mitano ya kifo cha Dokta. Sengondo Mvungi, aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, kongamano lililoandaliwa na kituo cha haki za binadamu (LHRC) na jumuiya ya wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udasa).

Akizungumza katika kongamano la kutimiza miaka mitatu tangu aingie madarakani rais wa Tanzania, John Magufuli alisema anafahamu hitaji la watanzania kuhusu katiba mpya lakini si kipaumbele chake kwa sasa.

"Ninashauri tuendelee kuzungumza,Kumuomba Mungu na kushauriana ili tupate katiba mpya kwa sababu katiba mpya ndio msingi wa kuendesha nchi,"amesema Butiku ambaye alihudumu kwa nafasi mbalimbali katika serikali ya awamu ya kwanza.