KENYA-JAMII-HAKI

Wanawake waamua kubeba ujauzito kwa niaba ya wanawake tasa, kwa kukidhi mahitaji yao Kenya

Nchini Kenya, wanawake wanaojiuza miili yao huchangia kwa karibu 15% katika maambukizi mapya ya VVU.
Nchini Kenya, wanawake wanaojiuza miili yao huchangia kwa karibu 15% katika maambukizi mapya ya VVU. Georgina Goodwin / AFP

Wanawake nchini Kenya wameanza kufanya kazi ya kujitolea kubeba ujauzito kwa niaba ya wanamke waoleaji ambao ni tasa japo kwa masharti, katika juhudi za kutafuta ajira pamoja na kupambana na hali mbaya ya uchumi nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Iren Kerubo ni Mama wa watoto wawili, ambaye anayeishi mjini Mombasa, anasema ameamua kujihusisha na biashara hii baada ya kutafuta ajira kwa muda bila mafanikio, biashara ambayo anasema aliifahamu kupitia mitandao ya kijamii.

“Niliingia kwenye mtandao nikatafuta, nikapata nikajisajili, tuseme kama mtu uko na mzee wako unaishi naye na pengine  katika miaka mingi unatafuta mtoto na haujampata, kwa hiyo nachukuwa uamuzi wa kufanya kazi hiyo ili niweze kukidhi maisha, “ Iren Kerubo amesema.

Ni biashara ambayo haijakuwa na umaarufu hapa nchini lakini kwa Iren, imekuwa ikiendelea kwa siri, japo kuna mikataba ya kisheria ambayo inafaa kuzingatiwa baina yake na familia ambayo haiwezi kupata mtoto.

“Ukiwa umebeba mimba kwa miezi Tisa kuna makubaliano, wale wazazi watakuwa na mwanasheria wao na mimi nitakuwa na wangu, yule mtoto sidhani kama nitatamani kwenda naye, kwani niko na wangu wananitosha, katika mchakato huo, sitakuwa uhusiano wowote na yule mtoto,” ameongeza Iren Kerubo.

Lakini viongozi wa dini wanapinga hali hiyo na kusema kuwa sasa jamii ina jinamizi ambalo watu kupata madhambi makubwa, huku wakionya waumini wa dini mbalimbali kufanya matendo mesma ambayo hayatomkasirisha Mungu.

“Ni jambo ambalo limeanza kuja sehemu za kwetu na ni jambo ambalo pia tunahitaji watu wajichunge, manake kuna wale  ambao wanafanya hivyo kutunga mimba watoto wa kwenda kuuza, hilo hatuwezi kulikubali” amesema Martin Kivuva, askofu mkuu wa jimbo la Mombasa.

Gunga Mwinga. Mwanasheria nchini Kenya, anasema suala hili bado ni nyeti  nchini humo kutokana na maadili ya jamii, japo kunafaa kuwa na mkataba wa kisheria baina ya pande zote mbili.

“Ni swala ambalo ni jipya, halijaweza kuingia sana katika akili za binadamu hasa katika Jamuhuri yetu ya  Kenya,” amesema Bw Mwinga

Hata hivyo raia nchi Kenya ambao waliweza kuongea na Idhaa ya Kiswajili ya RFI wanasema swala hili haliambatani na maadili ya jamii na ni la kupotosha.

Ripoti ya Mwandishi wetu wa Mombasa, Joseph Jira