UGANDA-ZIWA VICTORIA-AJALI-MAUAJI

Ajali: Watu zaidi ya 10 wapoteza maisha Ziwa Victoria nchini Uganda

Ziwa Victoria
Ziwa Victoria COURTESY PHOTO

Watu zaidi ya 10 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 40 wameokolewa, baada ya boti waliyokuwa wanasafiria kuzama katika Ziwa Victoria nchini Uganda.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, kuna hofu kuwa idadi kubwa ya watu hawajaonekana kwa mujibu wa ripoti za polisi.

Aidha, haijafahamika, boti hiyo ilikuwa na abiria wangapi.

“Kikosi chetu cha uokozi, kimewaokoa watu 40 wakiwa hai. Zoezi hilo linaendelea,” amesema msemaji wa Polisi Emilian Kayima.

Haijafahamika, kilichosababisha kuzama kwa boti hiyo.

Miezi miwili iliyopita, watu zaidi ya 200 walipoteza maisha katika nchi jirani ya Tanzania baada ya kuzama kwa Ferry katika kisiwa hicho, katika Ziwa hilo ambalo linamilikiwa na nchi za Afrika Mashariki ya Kenya, Uganda na Kenya.