TANZANIA-JOHN MAGUFULI-UTAWALA BORA

Rais Magufuli: Wanasiasa wa upinzani watulie la sivyo wataishia magerezani

Rais wa Tanzania, John Magufuli
Rais wa Tanzania, John Magufuli afrinews.com

Rais wa Tanzania, John Magufuli amesema wanasiasa wa upinzani wanapaswa kutulia la sivyo wataishia magerezani.

Matangazo ya kibiashara

Magufuli, rais wa Tanzania tangu mwaka 2015 ametoa matamshi hayo katika uzinduzi wa maktaba ya kisasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo Novemba 27, Maktaba hiyo imejengwa kwa msaada wa serikali ya China, katika hafla iliyohudhuriwa na viongozi na wanasiasa mbalimbali akiwemo Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa.

Kabla ya kutoa kauli hiyo, rais Magufuli alimsifu Wazieri Mkuu wa zamani Edward Lowassa kuwa ni mwanasiasa mstaarabu ambaye alionyesha utulivu hata baada ya kushindwa katika uchaguzi wa 2015.

Uchaguzi wa 2015, uligombewa kwa udi na ubani na Magufuli ambaye aliibuka mshindi kwa kura zaidi ya milioni 8 huku Lowassa ambaye aliwania kupitia C hadema na kuungwa mkono na vuama vingine vya siasa chini ya mwavuli wa Ukawa akivuna kura zaidi ya milioni 6.

"Nakupongeza sana Lowassa, vyama vyetu visiwe chanzo cha kututenganisha bali viwe chachu ya kuleta maendeleo. Nimezungumza hili kwa heshima kubwa ili ukawashauri wale unaowaongoza watulie vinginevyo wataishia magereza,"amesema kiongozi huyo.

Kauli ya Magufuli inakuja wakati huu Tanzania ikishuhudia wanasiasa wa upinzani wakibaliwa na mashtaka katika mahakama za Tanzania.

Wiki iliyopita Kiongozi wa Chama kikuu cha Upinzani Chadema, Freeman Mbowe na mbunge wa Tarime Mjini Easther Matiku walifutiwa dhama ma kutokana na kukiuka masharti ya dhamana katika kesi inayowakabili ya kufanmya mikusanyiko kinyume cha sheria.

Aidha, kiongozi mwingine wa upinzani Zitto Kabwe, anakabiliwa na mashtaka ya uchochjezi katika mahakama ya Kisutu.

,aktaba ya kisasa iliyozinduliwa inaweza kuchukua kwa wakati mmoja watu 2100 na kutunza vitabu 800,000.