KENYA-USALAMA

Zoezi la kumtafuta raia wa italia aliyetekwa nyara Chakama laendelea

Helikopta ya jeshi la Kenya ikishiriki katika zoezi la kumtafuta raia wa Italia aliyetekwa nyara Kusini Mashariki mwa nch hiyo.
Helikopta ya jeshi la Kenya ikishiriki katika zoezi la kumtafuta raia wa Italia aliyetekwa nyara Kusini Mashariki mwa nch hiyo. REUTERS/Gregory Olando

Ni wiki moja sasa tangu zoezi la kumtafuta Silvia Romano, raia wa Italia aliyetekwa nyara katika soko la Chakama, Kaunti ya Kilifi, Kusini Mashariki mwa Kenya lianze.

Matangazo ya kibiashara

Romano, mwenye umri wa miaka 23, alikua akifanya kazi ya kujitolea kuwasaidia watoto kutoka jamii ziosizojiweza katika shirika lisilo kuwa la kiserikali la Africa Milele Onlus.

Raia kwa upande wao wanaiomba serikali kuu nchini Kenya kufanya mbinu zote kuhakikisha Silvia Romano anapatikana akiwa hai.

Tayari watu ishirini wanaoshtumiwa katika utekaji nyara huo wamekamatwa.

"Watu wanaoshikiliwa na polisi tayari wametupa taarifa muhimu. Wattekaji nyara bado hawajajulikana, lakini tutajitahidi kwa njia zote zinazowezekana kumpata haraka mateka huyo, Mkuu wa polisi nchini Kenya Joseph Boinett amesema.

Hati ya kutafuta watuhumiwa watatu ilitolewa, huku serikali ikitenga kitita cha dola 30,000 kwa mtu atakaye toa taarifa yoyote itakayowezesha kuwakamata washtumiwa hao. Mke wa mmoja wa watuhumiwa hao pia anashikiliwa na polisi baada ya kupata mazungumzo kati yake na mumewe anayetafutwa.

Hakuna kundi lolote ambalo limedai kuhusika na utekaji nyara huo, Lakini kundi la Al shabab linashukiwa kuendesha kitendo hicho.