SUDANI KUSINI-UN-HAKI

Ubakaji dhidi ya wanawake Sudan Kusini: Umoja wa Mataifa walaani

Jimbo la Bentiu, limeendelea kuwa miongoni mwa maeneo hatari nchini Sudan Kusini ambayo wanawake wamekuwa wakishambuliwa na kubakwa.
Jimbo la Bentiu, limeendelea kuwa miongoni mwa maeneo hatari nchini Sudan Kusini ambayo wanawake wamekuwa wakishambuliwa na kubakwa. AFP PHOTO/Ivan LIEMAN

Umoja wa Mataifa umelaani vitendo vya kubakwa kwa wanawake na wasichana 125 katika jimbo la Bentiu hivi karibuni, nchini Sudan Kusini. Kulingana na shirika la Madaktari wasiokuwa na mipaka, MSF, kwa muda wa siku 10 zilizopita, wanawake na wasichana 125, wamebakwa nchini Sudan Kusini.

Matangazo ya kibiashara

Umoja huo umesema kitendo hicho hakikubaliwi katika eneo hilo ambalo linadhibitiwa na wanajeshi wa serikali.

Madakatari wasiokuwa na mipaka, MSF walisema kuwa wanawake na wasichana hao walibakwa wakati walipokwenda kuchukua chakula cha msaada katika jimbo la Bentiu, lakini viongozi wa eneo hilo wamekanusha madai hayo.

Jimbo la Bentiu, limeendelea kuwa miongoni mwa maeneo hatari nchini Sudan Kusini ambayo wanawake wamekuwa wakishambuliwa na kubakwa wakati wa vita kati ya makundi ya waasi na wanajeshi wa serikali.