SUDANI KUSINI-UN-HAKI

Udhalilishaji wa kingono Sudan Kusini: Umoja wa Mataifa waomba sheria ifaute mkondo wake

Jimbo la Bentiu, limeendelea kuwa miongoni mwa maeneo hatari nchini Sudan Kusini ambayo wanawake wamekuwa wakishambuliwa na kubakwa.
Jimbo la Bentiu, limeendelea kuwa miongoni mwa maeneo hatari nchini Sudan Kusini ambayo wanawake wamekuwa wakishambuliwa na kubakwa. AFP/SIMON MAINA

Umoja wa Mataifa unasema kuwa, zaidi ya wanawake na wasichana 150 wamejitokeza kwa kipindi cha siku 12 zilizopita, kyatafuta msaada wa kupewa matibabu baada ya kubakwa na wengine kudhulumiwa kingono.

Matangazo ya kibiashara

Awali shirika la Madaktari wasiokuwa na mipaka, MSF, lilisema kwa muda wa siku 10 zilizopita, wanawake na wasichana 125, wamebakwa nchini Sudan Kusini.

Mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa yanayotoa misaada ya kibinadamu nchini humo, yamesema kuwa wanawake na wasichana hao wamewataja watu wenye silaha, waliovalia mavazi ya kijeshi kuhusika.

Mark Lowcock, Mkuu wa misaada kutoka Umoja wa Mataifa kwa Sudan Kusini, amesema wanawake na wasichana hao wamedhulumiwa wakati wakienda kupokea chakula cha mssada katika mji wa Bentiu.

Jimbo la Bentiu, limeendelea kuwa miongoni mwa maeneo hatari nchini Sudan Kusini ambayo wanawake wamekuwa wakishambuliwa na kubakwa wakati wa vita kati ya makundi ya waasi na wanajeshi wa serikali.