Pata taarifa kuu
EAC-ZANZIBAR-UTENGAMANO

Spika wa bunge la Afrika Mashariki azuru Zanzibar

Spika wa bunge la Afrika Mashariki, Martin Ngoga (kushoto)akiwa na Spika wa baraza la wawakilishi Zuberi Maulid
Spika wa bunge la Afrika Mashariki, Martin Ngoga (kushoto)akiwa na Spika wa baraza la wawakilishi Zuberi Maulid Baraza la wawakilishi
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 1

Spika wa bunge la Afrika mashariki, Dr. Martin Ngoga amezuru Viswani Zanzibar kwa kutembelea taasisi mbalimbali zilizopo visiwani humo.

Matangazo ya kibiashara

Ziara hiyo inakuja kwa lengo la kutekeleza majukumu  yake ya mtangamano na kuimarisha mahusiano baina ya bunge la Afrika Mashariki na taasisi mbalimbali.

Zanzibar, inahodhi makao makuu ya kamisheni ya Kiswahili ya Afrika Mashariki, taasisi yenye wajibu wa kuimarisha lugha ya Kiswahili katika nchi wanachama.

Aidha Spika Ngoga aliyeambatana na viongozi mbalimbali wakiwemo wabunge wa bunge la Afrika masharik, Dr Abdullah Makame ambaye ni mwenyekiti wa wabunge wa tanzania katika bunge la EAC, pia amezuru baraza la wawakilishi  na kukutana na Spika wa baraza hilo, Zuberi Maulid.

Bunge la Afrika mashariki liliundwa kupitia mkataba wa 1999, kikiwa ni chombo cha kutunga sheria zinazotumika katika nchi wanachama.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.