Pata taarifa kuu
AFRIKA-HAKI ZA BINADAMU-TANZANIA

Balozi Ufaransa: Sanaa inasaidia kuelimisha jamii kuhusu haki za binadamu

Naibu balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Alexandre Peaudeau
Naibu balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Alexandre Peaudeau RFI/Fredrick Nwaka
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 5

Ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania umesema sanaa ya michoro inaweza kusaidia kufikisha ujumbe kwa jamii kuhusu haki za binadamu.

Matangazo ya kibiashara

Kaimu balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Alexandre Peaudeau ametioa kauli hiyo jana wakati akizungumza katika hafla ya kuadhimisha miaka 70 tangu lilipotolewa tamko la haki za binadamu, tukio lililofanyika katika kituo cha utamaduni cha Ufaransa Jijini Dar es salaam.

"Sanaa ya michoro inasaiadia kutoa ujumbe kwa jamii na hususani ni vijana kutambua haki na wajibu wao kama unavyoainisha mkataba wa haki za binadamu.

Hafla hiyo ilifanyika katika kituo cha utamaduni cha Ufaransa Alliance Francaise ambapo Naibu Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Alexandre Peaudeau amesema maudhui inayotumia sanaa husaidia taifa kutambua haki za msingi za binadamu.

FREDRICK NWAKA WRAP ON HAKI ZA BINADAMU 11 DEC 2018

Kwa upande wake balozi wa Ubelgiji nchini Tanzania Peter Van Acker ametoa wito kwa mamlaka za Tanzania kudumisha ulinzi wa haki za bindamu wakati huu dunia ikiadhimisha siku ya haki za binadamu.

Baadhi ya wananchi waliohudhuria halfa hii na kuzungumza na idhaa hii walieleza kufurahishwa na maudhui yaliyoandaliwa na ubalozi wa Ufaransa kuadhimisha siku ya Haki za Binadamu, wengi wakikubaliana na ukweli kuwa sanaa ya uchoraji ikitumika vizuri inaweza kuhamasisha jamii kwa maendeleo na kutambua haki zao.

Mapema kabla ya tukio hilo wanafunzi wa shule za msingi na sekondari walifundishwa matumizi ya sanaa katika kutambua haki na wajibu wao kama ambayo mkataba wa haki za binadamu ulivyoainisha.

Mbali na balozi Peaudeau pia hafla hiyo ilihudhuriwa na balozi wa ubelgiji nchini Tanzania, Peter Van Ackerm wanadiploamsia mbalimbali na waandishi wa habari.

Habari hii imeandikwa na mwandishi wetu Fredrick Nwaka.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.