RWANDA-DRC-FDLR

Wanajeshi wawili wa Rwanda wauawa baada ya kushambuliwa na waasi wa FDLR

Waasi wa FDLR
Waasi wa FDLR AFP/ Lionel Healing

Wanajeshi wawili wa Rwanda wameuliwa na waasi waliovuka mpaka kutoka nchini DRC na kuwashambulia.

Matangazo ya kibiashara

Rais Paul Kabgame, amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo, ambayo anasema yametekelezwa na waasi wa FDLR.

“Kundi la waasi kutoka DRC lilivamia ngome zetu, nafikiri waliwauwa wanajeshi wetu wawili au watatu,” alisema rais Kagame.

Hata hivyo, Kagame amesema kuwa baadhi ya waasi hao waliuawa baada ya kushambuliwa na wanajeshi wa Rwanda.

“Idadi kadhaa ya waasi hao waliuawa na miili yao kupelekwa na marafiki zao nchini DRC. Tunaendelea kuwasiliana na DRC,” aliongeza.

Waasi wa FDLR, wameendelea kushtumiwa kuhusika pakubwa katika mauji ya kimbari nchini Rwanda mwaka 1994 na baadaye kukimbilia Mashariki mwa DRC ambako pia, wameendelea kushtumiwa kutekeleza mauaji dhidi ya raia na wanajesji wa taifa hilo.