TANZANIA-VYAMA VYA SIASA-KATIBA

Kesi ya kupinga muswada wa vyama vya siasa yarindima Tanzania

Zitto Kabwe (wa tatu kutoka kushoto) akiwa na wanasiasa wengine katika mahakama ya Tanzania Jijini Dar es salaam, Tarehe 4 Januari 2019
Zitto Kabwe (wa tatu kutoka kushoto) akiwa na wanasiasa wengine katika mahakama ya Tanzania Jijini Dar es salaam, Tarehe 4 Januari 2019 RFI/Fredrick Nwaka

Kesi namba 31 ya kupinga muswada wa sheria mpya ya vyama vya siasa imesikilizwa kwa mara ya kwanza leo katika mahakama kuu ya Tanzania, masijala ya Dar es Salaam.

Matangazo ya kibiashara

Kesi hiyo imefunguliwa na Zitto Kabwe, akiwakilisha wafungua maombi wengine wawili wakiitaka mahakama ya Tanzania kuzuia bunge lisijadili muswada huo.

Hata hivyo Kesi hiyo imeahirishwa hadi Januari 11 ili kutoa fursa kwa mawakili wa upande wa serikali kujibu maombi yaliyowasilishwa kupinga muswada huo. Januari 11 hiyohiyo mahakama itatoa uamuzi wake kuhusu maombi yaliyowasilisha mahakamani hapo.

Wawasilisha maombi wanasema ikiwa muswada huo utajadiliwa na kupitishwa kuwa sheria, utazuia vyama vya siasa kufanya shughuli zao na kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya chama kimoja cha siasa.

Mwandishi wa RFI Kiswahili Fredrick Nwaka mapema leo alifika mahakamani kushuhudia usikilizwaji wa kesi hiyo na anasema kesi hiyo imezua joto la kisiasa nchini Tanzania.