UGANDA-USALAMA

Waziri wa Sudan Kusini akamatwa akivuta sigara hadharani Uganda

Mji mkuu wa Uganda, Kampala.Tangu mwaka 2016, Uganda imekuwa ikitekeleza sheria ya kupiga marufuku uvutaji wa sigara hadharani.
Mji mkuu wa Uganda, Kampala.Tangu mwaka 2016, Uganda imekuwa ikitekeleza sheria ya kupiga marufuku uvutaji wa sigara hadharani. REUTERS/James Akena/File Photo

Watu kumi na saba akiwemo Waziri kutoka Sudan Kusini wamekamatwa jijini Kampala, mji mkuu wa Uganda kwa madai ya kuvuta sigara hadharani.

Matangazo ya kibiashara

Polisi jijini Kampala wamethibitisha ukamatwaji huo, lakini wamemwachilia huru Waziri huyo wa nchi jirani ya Sudan Kusini.

Ripoti zinasema, hatapelekwa Mahakamani ili kuzuia mvutano wa kidiplomasia kati ya Kampala na Juba.

Tangu mwaka 2016, Uganda imekuwa ikitekeleza sheria ya kupiga marufuku uvutaji wa sigara hadharani.