KENYA-USALAMA

Kenya: Hoteli ya kifahari yashambuliwa Nairobi

Magari yakiwaka moto mbele ya hoteli kubwa ya kifahari ya Dusit iliyolengwa na shambulizi Nairobi, Kenya, Januari 15, 2019.
Magari yakiwaka moto mbele ya hoteli kubwa ya kifahari ya Dusit iliyolengwa na shambulizi Nairobi, Kenya, Januari 15, 2019. © REUTERS/Thomas Mukoya

Hoteli kubwa ya kifahari katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi imeshambuliwa Jumanne hii Januari 15, 2019. Kwa mujibu wa mashahidi, kulisikika milipuko miwili mikubwa ikifuatiwa na risasi nyingi.

Matangazo ya kibiashara

Kwenye mitandao ya kijamii, picha zinaonyesha moshi mkubwa ukifumba jengo hilo. Kundi la Al Shabab limekiri kuhusika na shambulio hilo.

Vikosi vya usalama vimepiga kambi katika eneo la tukio.

Shambulio hilo limetokea katika eneo la 14 Riverside Drive huko Westlands, mjini Nairobi, na limelenga hoteli ya kifahari ya DusitD2.

Watu kadhaa wamejeruhiwa na wanahudumiwa na maafisa wa Shirika la Msalaba Mwekundu wakisaidia na watu wengine wa kujitolea.

Kenya imeendelea kutishiwa na magaidi wa Al Shabab kutoka Somalia, baada ya kutuma wanajeshi wake nchini humo mwaka 2011.