BURUNDI-EAC-USALAMA-SIASA

Burundi yajiandaa kushiriki Mkutano wa 20 wa EAC Arusha

Burundi imethibitisha kushiriki katika mkutano wa 20 wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, utakaofanyika mjini Arusha nchini Tanzania tarehe 1 mwezi Februari.

Rais Pierre Nkurunziza hajashiriki mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya kukosewa kupinduliwa mamlakani. 2018.
Rais Pierre Nkurunziza hajashiriki mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya kukosewa kupinduliwa mamlakani. 2018. REUTERS/Evrard Ngendakumana
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo uliahirishwa toka mwezi Novemba mwaka uliopita, baada ya Burundi kutotuma mwakilishi, ikidai kuwa ilisusia kwa sababu ya tufauti zake na jirani yake Rwanda.

Hata hivyo, msemaji wa rais Pierre Nkurunziza , Jean Claude KAREGWA sasa amesema nchi hiyo iko tayari kushiriki katika mkutano huo.

Mkataba uliounda jumuiya hiyo ambayo ina nchi sita, hauwezi kufanyika ikiwa nchi moja haitatuma mwakilishi wake katika mkutano mkuu.