RWANDA-USALAMA

Kumi na nne wapoteza maisha katika maporomoko ya mgodi Rwanda 

Wilaya ya Rubavua mbako kunapatikana moja ya migodi nchini Rwanda.
Wilaya ya Rubavua mbako kunapatikana moja ya migodi nchini Rwanda. AFP PHOTO / STEPHANIE AGLIETTI

Watu 14 wamepoteza maisha Mashariki mwa Rwanda, baada ya mgodi kuporomoka. Mashahidi wanasema kuna uwezekano kuwa idadi hiyo ikaongezeka kutokana na kuwa kuna watu wengine ambao waliokoloewa wakiwa katika hali mbaya.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti za serikali zinasema kuwa, wanawake saba ni miongoni mwa watu waliopoteza maisha.

Jean Claude Rwagasana, mwakilishi wa serikali katika eneo la Mwulire amesema, mgodi huo uliporomoka wakati wachimba migodi hao walipokuwa kazini.

Walikuwa wanachimba madini aina ya cassiterite. Mwaka 2017 wachimba migodi 27 walipoteza maisha katika janga kama hili.

Mamlaka ya udhibiti wa madini imekuwa ikishutumu mara kwa mara kampuni ya madini kuhusika na vifo hivyo, ikibaini kwamba migodi mingi haikuandaliwa ipasavyo  na kwamba makampuni katika sekta hiyo wameshindwa kutekeleza hatua za usalama kwa wachimba migodi.