RWANDA-HAKI-SIASA

Rwanda yatoa waranti wa kimataifa wa kukamatwa Kayumba Nyamwasa

Jenerali Faustin Kayumba Nyamwasa wakati kesi yake katika mahakama Johannesburg Julai 10, 2012.
Jenerali Faustin Kayumba Nyamwasa wakati kesi yake katika mahakama Johannesburg Julai 10, 2012. AFP PHOTO / STEPHANE DE SAKUTIN

Serikali ya Rwanda imetoa waranti kadhaa za kimataifa kufuatia mashambulizi ya hivi karibuni kusini mwa Rwanda. Miongoni mwa Waranti hizo wapo wafuasi wa chama cha P5 na Jenerali alieasi Kayumba Nyamwasa.

Matangazo ya kibiashara

P5 ni jukwaa la vyama vya kisiasa vya upinzani nchini Rwanda ambavyo vinatuhumiwa kuanzisha uasi mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo dhidi ya serikali ya Rwanda, jambo ambalo limekuwa likikanushwa na jukwaa la vyama hivyo. Mwezi Julai mwaka jana, vyama hivyo viliomba kuandaliwa kwa mazungumzo ya kisiasa na rais Paul Kagame, ombi ambalo mpaka sasa halikupata jibu.

Jenerali Kayumba Nyamwasa, mkuu wa zamani wa majeshi ya Rwanda ni miongoni mwa watu wanaohusika na waranti hizo za kimataifa.

Jenerali Nyamwasa alikuwa mtu wa karibu sana na rais Paul Kagame ambae kwa sasa anaeshi nchini Afrika Kusini chini ya ulinzi mkali wa idara ya usalama nchini humo baada ya jaribio la kutaka kuuwawa mwaka 2010.

Kiongozi huyo wa chama cha upinzani cha RNC pamoja na vyama vingine wanatuhumiwa na utawala wa Kigali kuanzisha uasi mashariki mwa Congo katika eneo la Fizi na Uvira. Serikali ya Kigali imetaka Pretoria Kumkamata Nyamwasa na kuzuia mali zake. Waranti hizo zimetolewa katika kipindi hiki kisichokuwa cha kawaida kati ya Rwanda na Congo na kati ya Rwanda na Afrika Kusini.