TANZANIA-MAZINGIRA-UFARANSA-MDAHALO

Plastiki zinachangia kupunguza Kuzaliana kwa Samaki Baharini

Kituo cha Utamaduni cha Alliance Francais
Kituo cha Utamaduni cha Alliance Francais Imani Nathaniel

Kutoridhiwa kwa Mkataba wa Mazingira na usimamizi wa Mali asili wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kumetajwa kuchangia kwa baadhi ya nchi Wanachama wa jumuiya hiyo kuchelewa kupiga marufuku matumizi ya plastiki na hivyo kuathiri mazingira.

Matangazo ya kibiashara

Hayo yamebainika katika Mdahalo wa usiku wa mawazo Uliowakutanisha wadau wa Mazingira, ulioandaliwa na Rfi na taasisi ya lugha za kifaransa katika nchi 70 Duniani.

Akifungua Mdahalo huo, Balozi wa Ufaransa nichini Tanzania Frederic Clavier anasema ni muhimu hatua kachukuliwa ili kuondokana na uchafuzi huo.

“ Tunazalisha Zaidi ya Tani Milioni 300 za Plastiki ,taka za plastiki kila Mwaka ambayo ni sawa na idadi ya watu waliopo Duniani kwa makadirio ni sawa na taka tani Bilioni 8.3 zimezalishwa tangu mwanzoni mwa miaka 1950”

Wakati tayari nchi za Rwanda na Kenya zimefanikiwa kupiga marufuku Matumizi ya Plastiki,Tanzania bado inasua sua licha ya kuwa na kiwango kikubwa cha uzalishaji wa taka za Plastiki, Mhandisi Viwanda kutoka ofisi ya makamu wa Rais Idara ya Mazingira Julius Moshi alisema wapo katika hatua za mwisho kuachana na matumizi ya plastiki kama vifungashio.

Kwa upande wake Mtafiti kutoka Chuo kikuu cha sayansi na tiba Muhimbili Hussein Mohamed ambae ni miongoni mwa wazungumzaji katika Mdahalo huo alisema Mbali na kuathiri mazalia ya samaki pia samaki ambacho ni chakula kuleta athari kiafya,na kusababisha uwekezano wa binadamu kupata magonjwa ya saratani,figo na athari katika via vya uzazi.

Tayari boti iliyotengenezwa nchini Kenya kwa kutumia plastiki imeanza safari yake kutoka Lamu Mombasa ikitarajia kufika Zanzibar zikiwa ni hatua ya Matumizi mbadala ya Plastiki zilizotumika ili kuondokana na uchafuzi wa Mazingira.

STEVEN MUMBI WRAP Kuhusu PLASTIKI 01 JAN 2019 PAD