KENYA-UCHUMI

Kenya kuanza kuuza mafuta

Kenya iligundua mafuta miaka saba iliyopita eneo la Turkanar kaskazini mwa Kenya.
Kenya iligundua mafuta miaka saba iliyopita eneo la Turkanar kaskazini mwa Kenya. © AFP/HO/Tullow Oil PLC

Kenya inaendelea na jitihada zake za kuzalisha mafuta ghafi. Kenya iligundua mafuta mnamo mwaka 2012 katika mkoa wa Turkana, kaskazini mwa nchi, kwa kiwango kilichokadiriwa sawa na mapipa milioni 560.

Matangazo ya kibiashara

Kenya ilianza kuzalisha mafuta mnamo mwezi Juni, na kuwa kwa mara ya kwanza nchi inayozalisha mafuta. Tangu wakati huo, Kenya inahifadhi bidhaa yake hiyo kwa kusubiri kuiuza na kuongeza kiwango

Tangu miezi minane iliyopita, malori yamekuwa yakisafirisha zaidi ya mapipa mia moja ya mafuta kwa siku kutoka Turkana.

Kufikia sasa, tayari Kenya imetoa mapipa 80,000 ambayo yanaendelea kuhifadhiwa kwenye matangi yaliyo mjini Lokichar

Kwa mujibu wa chanzo cha serikali, Kenya inatarajia kuongeza kiwango cha uzalishaji mnamo mwezi Mei, na hivyo kufikia mapipa 2,000 ambayo yatakuwa yakisafirishwa na malori. Visima vingine vya mafuta vitachimbwa na kufikia visma 300.

Hivi karibuni rais Uhuru Kenyatta alisema serikali yake imeweka mikakati ya kisheria, kuhakikisha kwamba wakati bidhaa hiyo itaanza kuuzwa, haitakuwa "laana" wala kuleta mvutano kama ulioshuhudiwa katika baadhi ya nchi zilizogundua mafuta katika siku za karibuni.

Kenya imejiunga na Uganda na kuwa nchi ya pili ya Afrika Mashariki kuzalisha mafuta.