BURUNDI-AMISOM-USHIRIKIANO

Kundi la kwanza la askari wa Burundi waondoka Somalia

Askari wa kikosi cha Umoja wa Afrika Somalia (AMISOM) kutoka Burundi wakipiga kambi Mogadishu, Novemba 18, 2011.
Askari wa kikosi cha Umoja wa Afrika Somalia (AMISOM) kutoka Burundi wakipiga kambi Mogadishu, Novemba 18, 2011. REUTERS/Stuart Price

Bunge la Burundi limetupilia mbali uamuzi uliotolewa hivi karibuni na Tume ya Umoja wa Afrika ili kupunguza wanajeshi na wafanyakazi 1,000 wa AMISOM wa kikosi cha pekee cha Burundi.

Matangazo ya kibiashara

Wabunge kwenye bunge hilo wameitaka Serikali ya Burundi kukubali kuondolewa kwa askari wote wa Burundi waliopelekwa huko Somalia iwapo tume hiyo ya Umoja wa Afrika itaendelea kuzingatia uamzi wake huo.

Kundi la kwanza kati ya askari 1,000 wanaotakiwa kuondoka nchini Somalia waliondoka Alhamisi wiki hii.

Kwa upande wa serikali ya Burundi, kupelekwa kwa askari wake nchini Somalia ni katika hali ya kupata fedha.

Serikali ya Burundi imekuwa ikishtumiwa kukwepesha sehemu ya mishahara, inayolipwa kwa dola na ambayo kwa kiasi kikubwa inatolewa na Umoja wa Ulaya.

"Kutokana na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu na hali ya kisiasa nchini, ni aibu, chanzo cha kidiplomasia kimesema. Kuondoa askari elfu moja ni njia ya kuadhibu viongozi wa nchi hiyo".

Burundi ni ya pili kwa askari wengi nchini Somalia. Zaidi ya askari 5,000 wa Burundi wanahudumu katika kikosi cha Umoja wa Afrika nchini Somalia, AMISOM.