KENYA-UFARANSA-MAZINGIRA

Kikao cha kwanza cha mazingira cha UN kufanyika Kenya

Emmanuel Macron katika kikao cha mazingira cha One Planet Summit New York, Septemba 26, 2018. Rais wa Ufaransa pia yupo Nairobi kwa kikao hicho.
Emmanuel Macron katika kikao cha mazingira cha One Planet Summit New York, Septemba 26, 2018. Rais wa Ufaransa pia yupo Nairobi kwa kikao hicho. © REUTERS/Shannon Stapleton

Wawakilishi wa serikali, taasisi za kifedha, makampuni, mashirika yasio ya kiserikali wanakutana nchini Kenya Alhamisi hii, Machi 14 kwa kikao cha tatu cha mazingira cha Umoja wa mataifa na cha kwanza Afrika. Watu zaidi ya 4,000 wanatarajiwa kushiriki kikao hicho.

Matangazo ya kibiashara

Mfululizo huu wa mikutano uliozinduliwa na Ufaransa mnamo mwaka 2017 unalenga kutoa fedha kwa ajili ya kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Wakati Afrika inahusika kwa asilimia 4 tu ya uzalishaji wa gesi chafu duniani, asilimia 65 ya raia wake huathirika moja kwa moja na mabadiliko ya hali ya hewa.

Mbali na mazungumzo na vikao mbalimbali, sehemu moja ya mkutano huo itagubikwa na kusainiwa kwa mipango halisi kwa bara hilo. "Mkutano huo umewaleta pamoja wadau katika masuala ya uchumi ambao watachukuwa hatua," mmoja wa washiriki katika kiako hicho amebaini.

Matangazo mengi bado ni siri. Hata hivyo, inafahamika kwamba baadhi ya mikataba itasaidia miji mbalimbali ya Afrika kufikia nishati endelevu. Kutakuwa na miradi ya kuhifadhi ardhi iliyo hatarini, kutoa mafunzo kwa watafiti na kupambana dhidi ya ukataji miti.

Benki ya Dunia linatarajia kutoa mara mbili kiwango chake cha fedha kusaidia Afrika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.