BURUNDI-CNL-USALAMA

Wafuasi wa chama cha Agathon Rwasa waendelea kukamatwa Burundi

Kusajiliwa kwa chama kikuu cha upinzani cha Agathon Rwansa, CNL, nchini Burundi katikati mwa mwezi Februari, hakukubadili chochote kwa upande wa wafausi wake ambao wanaendelea kukamatwa kwa wingi.

Mji mkuu wa Burundi, Bujumbura
Mji mkuu wa Burundi, Bujumbura © AFP/Carl de Souza
Matangazo ya kibiashara

Wafuasi wa chama hicho waliamini kwamba baada ya kusajiliwa kwa chama chao, wapata afueni ya kutonyanyaswa au kukamatwa na vyombo vya dola.

Chama hiki kimpya cha Agathon Rwasa kimeeleza katika taarifa yake kwamba kwa sasa zaidi ya wafuasi wake hamsini wanazuiliwa jela tangu kusajiliwa rasmi kwa chama hicho Februari 14, 2019. Idadi hiyo imethibitishwa na baadhi ya vyombo vya habari huru ambavyo bado vinafanya kazi nchini Burundi.

Kila wakati, wafuasi wa Agathon Rwasa wanakamatwa- kwa makundi madogo ya watu watatu, wanne au watanona vijana wa chama tawala, CNDD-FDD, Imbonerakure, ambao wanafanya kazi ya vikosi vya usalama.

Kwa mujibu wa mashahidi, vijana hao ambao hubebelea marungu na wakati mwengine bunduki na grunedi wanafanya kazi hiyo usiku. Mara nyingi hulazimisha watu kufungua milango ya nyumba zao na kuanza kuwafanyia vitendo viovu.

Hata hivyo serikali au chama cha CNDD-FDD hawajasema chochote kuhusu madai hayo.