Pata taarifa kuu
UGANDA-USALAMA

Uganda yazindua zoezi la kusajili silaha zinazomilikiwa na raia

Serikali ya Uganda inasema watu wameendelea kumiliki silaha kinyume cha sheria.
Serikali ya Uganda inasema watu wameendelea kumiliki silaha kinyume cha sheria. REUTERS/Jorge Silva/File Photo
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Serikali ya Uganda imezindua kampeni ya kuzitambua silaha zinazotumiwa na taasisi za serikali na zile za kibinafsi lengo ikiwa ni kupambana na uhalifu unaotakana na matumizi ya silaha.

Matangazo ya kibiashara

Kati ya mwaka 2014 na 2016 watu zaidi ya 500 walipoteza maisha kwa sababu ya matumizi mabaya ya silaha.

Uganda imetajwa kuwa na idadi kubwa ya kesi za uhalifu wa kijinai unaotokana na matumizi ya silaha haramu katika nchi za Afrika Mashariki

Ripoti iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya ndani wa Uganda imebainisha kuwa watu takribani 503 waliuwawa kati ya mwaka 2014 na 2016, na wengine 1,477 walinusurika baada ya kupata majeraha makubwa ya risasi.

Hii haijumuishi idadi ya uhalifu uliotendeka miaka mitatu iliyopita hususan uhalifu dhidi ya watu wanaojulikana ikiwa ni pamoja na viongozi wa kidini wa Kiislam

Polisi nchini Uganda inasema ripoti ya uhalifu wa kijinai ya hivi karibuni inaonesha uhalifu umeongezeka kwa asilimia 20% katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Kutokana na hali hiyo, serikali imeunda kikosi cha kuhakikisha silaha zote zinatambuliwa na kusajiliwa ikiwa ni pamoja na zile zinazomilikiwa na watu binafsi ili endapo silaha zitatumika kufanya uhalifu iwe rahisi kuibaini, kwa mujibu wa Naibu Msemaji wa Polisi Uganda, Polly Namaye.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uganda, Abiga Kania, amekiri kuwa serikali inakabiliwa na changamoto kubwa lakini amesema kampeni ya kuzitambua bunduki itapelekea hali ya uhalifu inapungua

Kutokana na hali hiyo, uhalifu nchini Uganda umekuwa sugu na watu wengine wamekuwa wakiingia nchini kupitia mipaka na hivyo kufanyiwa ukatili..

Fred Egesa ambaye ni mtaalam wa usalama amesema kampeni hiyo inaweza isisaidie kuondokana na uhalifu

Mbali na vyombo vya Usalama vya serikali, Uganda inaruhusu watu binafsi kumiliki silaha.

Inakadiriwa silaha 400,000 zinamilikiwa na raia, huku zilizosajiliwa kihalali ni 3,000 tu.

Wananchi wa Uganda wanasubiri hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Julai kujuwa silaha ngapi zitakua zimesajiliwa.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.