RWANDA-USALAMA

Rwanda yadai kumshikilia kiongozi wa waasi Callixte Nsabimana

Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Richard Sezibera, mamlaka ya upelelezi (RIB) wamethibitisha kukamatwa kwa Callixte Nsabimana, ambaye anajinasibu Callixte "Sankara", naibu kiongozi wa kundi la waasi la Rwandes Movement for Democratic Change ( MRCD) na msemaji wa tawi lake la kijeshi la FNL

Shirika la upelelezi la Rwanda Rwanda Investigation Bureau (RIB) lilithibitisha katika taarifa yake kwamba Callixte Nsabimana anazuiliwa baada ya kukamatwa katika mazingira ambayo tatanishi.
Shirika la upelelezi la Rwanda Rwanda Investigation Bureau (RIB) lilithibitisha katika taarifa yake kwamba Callixte Nsabimana anazuiliwa baada ya kukamatwa katika mazingira ambayo tatanishi. RFI/Stéphanie Aglietti
Matangazo ya kibiashara

Kundi la FLN linadaiwa kutekeleza mashambulizi Kusini mwa Rwanda.

Vyombo kadhaa vya habari, hususan nchini Uganda, viliripoti katikati ya mwezi Aprili kukamatwa kwa mpinzani wa Rwanda Callixte Nsabimana ambaye anafahamika kwa jina maarufu la Callixte "Sankara" ambaye alikuwa anatafutwa kwa miezi kadhaa na serikali ya Rwanda na ambaye alikuwa analengwa na waranti tangu mwanzoni mwa mwaka huu.

Wiki mbili baadaye, tarehe 30 Aprili, shirika la upelelezi la Rwanda Rwanda Investigation Bureau (RIB) lilithibitisha katika taarifa yake kwamba Callixte Nsabimana anazuiliwa baada ya kukamatwa katika mazingira ambayo tatanishi.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Richard Sezibera pia alithibitisha taarifa hiyo katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumanne, bila kutoa maelezo zaidi kuhusu jinsi alivyokamatwa.