TANZANIA-JAMII

Bilionea wa Tanzania Reginald Abraham Mengi afariki dunia

Reginald Abraham Mengi alizaliwa mwaka 1944 mkoani Kilimanjaro.
Reginald Abraham Mengi alizaliwa mwaka 1944 mkoani Kilimanjaro. eastafricatv.twitter.com

Nchini Tanzania, Mwenyekiti wa makampuni ya IPP na moja ya watu matajiri na mashuhuri nchini Tanzania Reginald Abraham Mengi amefariki dunia. Taarifa hiyo imethibitishwa leo alfajiri na vyombo vya habari vilivyo chini ya umiliki wake, runinga ya ITV, na stesheni ya Radio ONE

Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kuwa amefariki akiwa mjini Dubai. Mwaka uliopita, alichapisha kitabu cha maisha yake “I Can, I Must, I Will”.

Mzee Mengi alizaliwa mnamo mwaka 1944 mkoani Kilimanjaro.

Kupitia kampuni yake hiyo Reginald Mengi aliweza kumiliki vyombo mbalimbali vya habari mfano kwa upande wa TV alimiliki ITV, EATV na Capital Tv na kwa upande wa Radio anamiliki Radio one, Capital radio na EATV radio. Dr. Reginald Mengi alimiliki magazeti kadhaa, mfano wa magazeti hayo ni Nipashe, kulikoni, Taifa letu , The Guardian , Financial time na Sunday observer.

Mwaka 1992 Dr. Mengi alianzisha makampuni mengi zaidi yaliyokuwa yanazalisha bidhaa mbalimbali za kawaida ambazo zilikuwa ni adimu sana kwa wakati huo. Alikuwa tayari anamiliki biashara kadhaa ambazo ni;- Tanzania Kalamu Company Limited, Anche-Mwedu Limited, Tanpack Industries Limited, Industrial Chemicals Limited ambacho baadaye ilibadili jina na kuitwa Bodycare Limited pamoja na Bonite Bottlers Limited.
Mwaka 1981 Dr. Mengi alianzisha kampuni kubwa ya uwekezaji iliyokwenda kwa jina la Mengi Associates Limited ambayo mwaka 1988 ilibadili jina na kuitwa Industrial Projects Promotion Limited na baadaye IPP Limited. IPP Limited kwa sasa ni jina linalojulikana sana Tanzania. Dr. Mengi anasema karibia fedha yote anayotumia kuanzisha makampuni haya inatokana na faida inayopatikana katika kampuni zilizopo.
Dr. Mengi alikuwa anasita sana kuwekeza katika vyombo vya habari kutokana na uhalisia wa mazingira ya kitanzania kisiasa lakini kufikia mwaka 1993 aliamua kuingia huko kwa kuanzisha Radio One, Itv kisha magazeti kama vile Nipashe, The Guardian n.k.
Reginald Mengi alimiliki viwanda baadhi ambavyo vinazalisha vinywaji mbalimbali hapa Tanzania. Alimiliki viwanda vya kutengeneza vinywaji, Bonite Bottlers inayoongoza kwa kinywaji cha Coca-Cola na maji ya chupa ya Kilimanjaro. Dr. Mengi pia amewekeza katika madini, mafuta, gesi, gesi asilia, madawa, kilimo cha mboga mboga katika maeneo makubwa, magari(kuunganisha magari ya umeme), saruji na mambo mengine zaidi katika sekta ya utengenezaji(manufacturing sector).

Dr. Mengi amewahi pia kuwa katika nafasi kadhaa za uongozi wa umma ikiwa ni pamoja na Mwenyekiti wa magazeti Tanzania(Chairperson of Tanzania Standard Newpapers); Kamishna wa kamati inayoshughulikia mishahara(Commissioner of Salary Review Commission); Mwenyekiti wa bodi ya Wahasibu na Wakaguzi Tanzania(NBAA); Mwenyekiti wa Baraza la Taifa La Mazingira Tanzania(National Environmental Council of Tanzania(NEMC); Mwenyekiti wa Vyombo vya habari vya Jumuia ya Madola Tanzania(Chairman of the Tanzania Chapter Commonwealth Press Union(CPU)); Mkurugenzi wa bodi ya LEAD(Leadership for Environment and Development International); Kamishna wa kamati ya Ukimwi Tanzania (Commissioner of Tanzania Commission for AIDS(TACAIDS); Mwenyekiti wa Muungano wa viwanda Tanzania(Chairman of the Confederation of Tanzania Industries(CTI); Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la Afrika Mashariki(Chairman of the East African Business Council); Mwenyekiti wa ICC Tanzania (a National Committee of the Intenational Chamber of Commerce); Na Mkurugenzi wa Bodi Ya Baraza la Biashara la Jumuiya ya Madola(Director of the Board of Commonwealth

Kuanzia mwaka 1987 Dr. Mengi amekuwa akisaidia upandaji miti kuzunguka mlima Kilimanjaro kwa sababu amekuwa akiona msitu ukipungua katika mlima Kilimanjaro. Mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka 2014 zaidi ya miti milioni 24 ilikuwa imepandw. Kwa mchango huu katika mazingira, Rais Mkapa alimchagua kuwa Mwenyekiti wa Baraza la kusimamia Mazingira Tanzania(NEMC)National Environmental Management Council licha ya kwamba anatokea katika sekta binafsi.
Dr. Mengi hadi mauti unamkuta alikuwa ni Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo Vya Habari Tanzania(Chairman of the Media Owners Association of Tanzania(MOAT) na Mwenyekiti wa Sekta Binafsi Tanzania(the Tanzania Private Sector Foundation (TPSF).Dr. Mengi alikuwa mtu anayejulikana sana kwa kutoa sana misaada ya kijamii(philanthropist). Amepewa tuzo mbalimbali kitaifa, kikanda na kimataifa akitambulika sana kwa kazi yake ya kujitolea kwa watu. Amepewa tuzo ya “The Order of the United Republic of Tanzania” mwaka 1994 na “The Order of The Arusha Declaration of the First Class” zilizotolewa na Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania mwaka 1995. Amepewa tuzo ya “The Martin Luther King Jr. Drum Major for Justice iliyotolewa na Marekani mwaka 2008. Amepewa tuzo ya “The International Order of the Lions Club iliyotolewa na Jumuiya ya Kimataifa ya Lions Club mwaka 2014; na “The 2012 Business For Peace Award” iliyotolewa na Taasisi ya Oslo Sweden ya “Business for Peace Foundation” baada ya kupendekezwa na kamati inayotoa tuzo za Nobeli.

Kwa kutambua juhudi zake za kupambana na rushwa na ufisadi nchini mwaka 2008 serikali ya Marekani ilimpatia tuzo ya “Martin Luther King Jr. Drum Major Award”.

Mengi amefariki dunia akiwa kwenye matibabu Dubai, U.A.E, usiku wa kuamkia leo.