TANZANIA-REGINALD MENGI-JOHN MAGUFULI

Rais John Magufuli aongoza watanzania kuaga mwili wa Reginald Mengi

Mamia ya raia wakiongozwa na rais wa Tanzania, John Magufuli wamejitokeza kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa mwenyekiti wa kampuni za IPP Dr Reginald Mengi aliyeaga dunia wiki iliyopita.

Rais John Magufuli akiwasili katika ukumbi wa Karemjee kuwaogoza watanzania kuaga mwili wa Dr Reginald Mengi tarehe 7 Mei 2019
Rais John Magufuli akiwasili katika ukumbi wa Karemjee kuwaogoza watanzania kuaga mwili wa Dr Reginald Mengi tarehe 7 Mei 2019 www.thecitizen.co.tz
Matangazo ya kibiashara

Tukio la kuaga mwili wa Mengi uliowasili jana kutoka Falme za kiarabu lilianza majira ya saa tatu asubuhi katika ukumbi wa Karemjee uliopo katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza kwa niaba ya serikali Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Profesa Palamagamba Kabudi amesema serikali imeguswa na kifo Dr. Reginald Mengi kutokana na mchjangop wake katika uchumi wa taifa.

Akizungumza kwa niaba ya wanadiplomasia waliopo Tanzania, balozi wa Ufaransa Frederick Clavier amesema kifo cha Mengi ni pigo kwa wadau wa maendeleo.

Wadau wa habari pia wamemzungumzia Reginald Mengi, Maxence Melo ni Mkurugenzi wa mtandao wa Jamii Forums anasema Mengi atakumbukwa kwa mema aliyoyatenda katika sekta ya habari.

Mwili wa Dr Reginald Mengi unatarajiwa kusafirishwa kesho kuelekea Moshi Mkoani Kilimanjaro kwa mazishi yatakayofanyika siku ya alhamisi.

Usikose kusikiliza matangazo yetu ya jioni