TANZANIA-MAFURIKO-DAR ES SALAAM

Mafuriko yaua watano Tanzania na kuwaacha maelfu bila makazi

Watu watano wamekufa na wengine zaidi ya 2500 hawana makazi wilayani kyela, kusini magharibi mwa Tanzania kutokana na mvua kubwa zinazonyesha nchini humo.

Athari za mvua zinazonyesha ni pamoja na kuharibika kwa miundombinu
Athari za mvua zinazonyesha ni pamoja na kuharibika kwa miundombinu The EastAfrican
Matangazo ya kibiashara

Katika wilaya ya kyela, eneo linalopakana na Malawi zaidi ya wakazi elfu mbili na mia tano hawana makazi kutokana na mvua kunyesha kwa wingi na kuharibu miundombinu.

Ripoti zilizochapishwa na shirika la habari la AFP zikimnukuu afisa wa wilaya Salome Magambo ni kwamba shule na huduma nyingine zimefungwa kutokana na mvua hizo.

Wilaya ya Kyela inapataka na ziwa Nyasa na nchi jirani ya malawi na ni mojawapo ya maeneo yanayopokea mvua nyingi nchini Tanzania.

Mapema wiki hii watu wawili waliripotiwa kupoteza maisha jijini Dar es Salaam kutokana na mvua kubwa zilizonyesha wiki hii.

Maeneo mengi nchini Tanzania ikiwemo ukanda  wa pwani kwa sasa yanashuhudia mvua kubwa huku wataalamu wa hali ya hewa katika taifa hilo wakionya mamlaka kuchukua tahadhari zaidi.