Rais John Magufuli mgeni rasmi mashindano ya kuhifadhi Quran
Imechapishwa:
Mashindano ya Kimataifa ya kuhifadhi Quran yanatarajiwa kutimuwa vumbi Jumapili hii Mei 19 jijini Dar es salaam nchini Tanzania, ambapo jumla ya washiriki 20 kutoka mataifa 18 wanashiriki.
Mshindi wa mashindano hayo atazawadiwa Milioni 20 za Tanzania.
Kwa mujibu wa waandaaji wa mashindano hayo taasisi ya Al Hikma Foundation mgeni rasmi anatarajiwa kuwa rais wa Tanzania, John Magufuli ambaye ataongoza viongozi mbalimbali wa serikali na dini katika tukio hilo litakalofanyika uwanja wa taifa Dar es Salaam.
Viongozi wengine wastaafu watakaohudhuria ni rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Tanzania, Jakaya Kikwete na Ally Hassan Mwinyi ambaye ni mlezi wa mashindano hayo.