KENYA-SOMALIA-DIPLOMASIA

Kenya yawazuia maafisa watatu wa Somalia kuingia nchini

Maafisa watatu wa serikali ya Somalia wamezuiwa kuingia nchini Kenya, baada ya kubainika kuwa hawakuwa na vibali vya kuingia katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

Abiria katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi
Abiria katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi PHOTO | COURTESY
Matangazo ya kibiashara

Gazeti la kila siku nchini humo la Daily Nation, linaripoti kuwa maafisa hao walikuwa wanakuja jijini Nairobi, kuhudhuria mkutano wa Umoja wa Ulaya kuhusu namna ya kuimarisha usalama mipakani.

Hatua hii imechukuliwa na maafisa wa nchi hiyo licha ya wawili hao kuripotiwa kuwa na pasi za kidiplomasia.

Gilbert Kibe Mkuruenzi wa mamlaka ya uwanja wa ndege nchini humo  amesema kuwa, hatua hiyo imechukuliwa kwa sababu za kiusalama.

Watatu hao wamebainika kwua Waziri wa Maji na Nishati Osman Libah, na wabunge Ilyas Ali Hassan nna Zamzam Dahir.

Maafisa wa uhamiaji wamewaambia maafisa hao kuwa walistahili kupata visa katika ubalozi wa Kenya mjini Mogadishu kabla ya safari.

Hivi karibuni, uhusiano wa Kenya na Somalia umekuwa mbaya kwa sababu ya mvutano kuhusu mmiliki wa eneo la Bahari Hindi.