RWANDA-UGAIDI-USALAMA

Callixte Nsabimana, akiri Mahakamani kuwa ni gaidi

Callixte Nsabimana, msemaji wa the National Liberation Front (FLN) Mei 23 2019
Callixte Nsabimana, msemaji wa the National Liberation Front (FLN) Mei 23 2019 http://www.therwandan.com/

Kiongozi wa waasi aliyeshutumiwa kutekeleza mashambulizi ya mauaji katika mikoa ya mpakani mwa Rwanda amepatikana na hatia ya kujihusisha na ugaidi na mashtaka mengine, na kukiri  kufanya kazi na serikali za kigeni dhidi ya Kigali.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hiyo ya Callixte Nsabimana, msemaji wa the National Liberation Front (FLN), inaweza kuongeza mvutano kati ya rais Paul Kagame na majirani zake wa karibu, ambao amekuwa akiwatuhumu kumchunguza.

Nsabimana alikamatwa mwezi uliopita kwa kujihusisha na kundi la FLN, wanaharakati waasi wanaolaumiwa kushambulia ndani ya Rwanda wakitokea eneo la misitu jirani na Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

“Naomba radhi kwa yote niliyofanya,” aliiambia Mahakama.

“Nataka kusema hapa wazi kuwa kazi yangu na kundi la FLN, imefika mwisho na chochote unachofanya kuanzia sasa hivi ni biashara yao, sio yao. Nawaomba radhi raia wote wa Rwanda.”

Wakili wake ameomba kuwa mteja wake amepewe dhamana na sasa kesi yake itasikilizwa siku ya Jumanne wiki ijayo.

Hata hivyo, kiongozi wa mashtaka, amepinga ombi kwa kile anachosema kuwa Nsabimana ni hatari na anaweza kutoroka.