KENYA-USHOGA-MAHAKAMA-KESI

Mahakama nchini Kenya yasisitiza ushoga na usagaji ni haramu

Mahakama Kuu nchini Kenya imetupilia mbali kesi ya wanaharakati wa mapenzi ya jinsia moja waliokuwa wanataka kubadilishwa kwa kifungu cha sheria inayoharamia mapenzi na vitendo vya jinsia moja nchini humo.

Wanharakati wa mapenzi ya jinsia moja nchini Kenya Mei 24 2019 wakiwa nje ya Mahakama jijini Nairobi
Wanharakati wa mapenzi ya jinsia moja nchini Kenya Mei 24 2019 wakiwa nje ya Mahakama jijini Nairobi www.reuters.com
Matangazo ya kibiashara

Majaji jijini Nairobi wamesema malalamishi wa wanaharakati hao haikuonesha ni namna gani sheria hiyo iliyotungwa wakati wa ukoloni inavyokwenda kinyume na katiba ya nchi hiyo na badala yake inatoa nafasi ya usawa kwa watu wote wanaoishi nchini humo.

Uamuzi huo wa Majaji hao watatu Roselyn Aburili, Chacha Mwita na John Mativo unamaanisha kuwa mapenzi ya jinsia moja yanasalia haramu nchini Kenya, kwa kile walichosisitiza kuwa sheria hiyo iko wazi na inamlinda kila mmoja.

Sheria hiyo inaeleza kuwa yeyote atakayeshatakiwa nchini humo kwa kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja, atahukumiwa jela miaka 14.

Muungano wa mashoga na wasagaji nchini humo unasema kuwa kumekuwa na kesi 15 dhidi wanachama wao mwaka 2018.

Uaumuzi huo uliotolewa siku ya Ijumaa, uliahirishwa kutoka mwezi Februari.

Kenya ni miongoni mwa mataifa mengi ya Afrika ambayo hayaungi mkono mapenzi ya jinsia moja licha ya shinikizo kutoka kwa mataifa ya kigeni.