Pata taarifa kuu
TANZANIA-EBOLA-AFYA-DRC-UGANDA

Tanzania yatoa tahadhari ya Ebola

Mtalaam wa Ebola
Mtalaam wa Ebola REUTERS/James Akena?
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Serikali ya Tanzania inasema imechukua tahadhari zote, kuhakikisha kuwa maambukizi ya ugonjwa hatari wa Ebola, hayaingii nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Tanzania inapakana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, nchi ambayo eneo la Mashariki limeathiriwa na ugonjwa huu ambapo watu zaidi 1,400 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 2,000 wameambukizwa.

Aidha, nchi hiyo inapakana na Uganda ambayo wiki iliyopita, mtoto mmoja na bibi yake waliokuwa wametokea nchini DRC walipoteza maisha wakipata matibabu katika Wilaya ya Kasese.

Waziri wa afya nchini humo Ummy Mwalimu, kupitia ukurasa wake wa Twitter ametoa tahadhari ya hatari ya maambukizi hayo kuingia nchini humo.

“Wizara ya Afya HAIJATANGAZA HALI YA HATARI bali tumetoa TAHADHARI KWA UMMA kuhusu Tishio la Ugonjwa wa Ebola ili wananchi wachukue hatua za kujikinga na kuhakikisha ugonjwa huu hauingii nchini kwetu,” aliandika.

Maeneo ambayo yapo kwenye hatari kubwa nchini humo ni pamoja na Kagera, Mwanza na Kigoma ambayo yanapana ana DRC na Uganda na tayari Waziri Mwalimu, ameanza ziara ya kuthathmini hali ilivyo katika maeneo hayo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.