SUDAN KUSINI-EU-VITA-MSAADA

Umoja wa Ulaya waipa Sudan Kusini msaada wa Euro Milioni 48.5

Wakimbizi wa ndani nchini Sudan Kusini
Wakimbizi wa ndani nchini Sudan Kusini AFP

Umoja wa Ulaya, umeipa Sudan Kusini Euro Milioni 48.5 kuisaidia kukabiliana na changamoto za kibinadamu zinazowakumbuka mamilioni ya raia wa nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Hii imekuja, baada ya Umoja wa Ulaya, wiki iliyopita, kutoka Dola Milioni 1.13 kuisadia nchi hiyo kupambana na maambukizi ya ugonjwa hatari wa Ebola.

Licha ya mkataba wa amani uliotiwa saini kati ya rais Salva Kiir na kiongozi wa upinzani Riek Machar mwaka 2018 baada ya mapigano tangu mwaka 2013, watu karibu milioni 2, wameyakimbia makwao na wengine Milioni saba wanahitaji misaada ya kibinadamu hasa chakula na dawa.

“Umoja wa Ulaya, unaeendelea kusimama na watu wa Sudan Kusini. Tunawakumbuka watu Milioni nne ambao wanaoishi kambini, na msaada huu utawasaidia kupata misaada mbalimbali,” amesema Christos Stylianides, anayehusika na misaada ya kibinadmau katika Umoja huo.

Fedha hizo pia zinatarajiwa kuwasaidia watu wenye uhitaji mkubwa kama watoto, wanawake na wazee ambao wanaishi kambini.

Tangu mwaka 2014, Umoja wa Ulaya umetoa Dola Milioni 623, kuwasaidia wananchi wa taifa hilo ambao wamekimbia makwao.