BURUNDI-BBC-VYOMBO VYA HABARI

BBC yaamua kufunga ofisi zake Burundi

Makao makuu ya BBC, London. BBC imeendelea kusisitiza kuwa makala iliyofanya na mwanaharakati wa Burundi yalifuata taratimu zote za kiuandishi na kutetea waandishi wake.
Makao makuu ya BBC, London. BBC imeendelea kusisitiza kuwa makala iliyofanya na mwanaharakati wa Burundi yalifuata taratimu zote za kiuandishi na kutetea waandishi wake. cc/Martin Leng

Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC limetangaza kufunga ofizi zake nchini Burundi pamoja na shughuli zake zote nchini humo baada ya juhudi za kupata suluhu na serikali ya burundi kukwama.

Matangazo ya kibiashara

Mwaka uliopita serikali ya Burundi ilipiga marufuku matangazo ya BBC na Sauti ya Amerika (VOA) ambapo serikali ilidai yamechafua sifa ya nchi.

Mwezi Maci mwaka huu Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, ilitoa wito kwa serikali ya Burundi, kubadilisha uamuzi wake wa kufungia matangazo ya Shirika la Utangazaji la Sauti ya Amerika (VOA) na BBC.

Msemaji wa Wizara hiyo Robert Palladino aliitaka serikali nchini humo pia kuwaruhusu wanahabari wanaofanya kazi na mashirika hayo, kuwaacha wafanya kazi yao kwa uhuru kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka ujao.

Burundi imechukua hatua hiyo kwa madai kuwa mashirika hayo ya kimataifa hayakufuata sheria zinazotoa muongozo wa uandishi habari nchini' na 'kukiuka maadili ya kikazi' na sheria za nchi hiyo kuhusu uanahabari.

Serikali ya Burundi inaishutumu BBC kwa kushindwa kumwajibisha mwanaharakati wa Burundi katika mahojiano na idhaa ya Kifaransa ya shirika hilo.

Serikali ya Burundi inasema kuwa ilichukua hatua hiyo ya kufunga matangazo ya BBC nchini kufuatia makala ya uongo ya shirika hilo mwaka uliopita kuhusu mauaji yaliotekelezwa na vikosi vya usalama katika nyumba ya siri ndani ya mji mkuu wa Bujumbura.

Hata hivyo BBC imeendelea kusisitiza kuwa makala hayo yalifuata taratimu zote za kiuandishi na kutetea waandishi wake.

Radio kadhaa za kibinafasi zimeharibiwa na kufungwa nchini humo wakati wa mzozo wa kisiasa uliozuka mnamo 2015, wakati rais Nkurunziza alipotangaza nia yake ya kuwania muhula wa tatu katika uchaguzi wa urais alioshinda baadaye mnamo mwaka 2015.

Tangu hapo, takribani watu 430,000 , wakiwemo wanasiasa wa upinzani wameitoroka Burundi.