KENYA-RUSHWA-UCHUMI-HAKI

Waziri wa fedha wa Kenya kufikishwa mahakamani

Henry Rotich, Waziri wa Fedha, aliyekamatwa kwa madai ya rushwa.
Henry Rotich, Waziri wa Fedha, aliyekamatwa kwa madai ya rushwa. REUTERS/Baz Ratner

Waziri wa fedha nchini Kenya Henry Rotich sambamba na watuhumiwa wengine kadhaa hii leo wanatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya hapo jana kukamatwa kwa amri ya mwendesha mashataka mkuu wa serikali kwa tuhuma za rushwa.

Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na wanahabari Jumatatu wiki hii, Mwendesha mashtaka mkuu Noordin Haji amesema kukamatwa kwa waziri huyo na wenzake kunatokanana uchunguzi walioufanya kuhusiana na makosa ya rushwa na matumizi mabaya ya fedha za uma, ukihusisha mamilioni ya dola za Marekani kuhusu ujenzi wa Mabwawa hewa.

Kukamatwa kwa Rotich ni mfululizo wa hatua ambazo zimeendelea kuchukuliwa na ofisi ya mwendesha mashtaka na mkurugenzi wa makosa ya jinai George Kinoti, ambao kwa pamoja waliapa kupambana vilivyo na russhwa nchini humo.

Rotich anashtakiwa sambamba na watuhumiwa wengine 27 ambao baadhi yao wanaendelea kusakwa na polisi.