Pata taarifa kuu
UGANDA-BOBI-ZIGGY-SIASA-USALAMA

Rafiki wa karibu wa Bobi Wine afariki dunia polisi yaanzisha uchunguzi

Ziggy Wine alitekwa wiki iliyopita na alipatikana Jijini Kampala siku tatu baadae (Jumamosi ya wiki iliyopita) akiwa ameng’olewa kucha na jicho moja.
Ziggy Wine alitekwa wiki iliyopita na alipatikana Jijini Kampala siku tatu baadae (Jumamosi ya wiki iliyopita) akiwa ameng’olewa kucha na jicho moja. BOBI WINE/Twitter.com
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Mwanamuziki Allinda Michael, maarufu kama Ziggy Wine, anayeshirikiana kwa kwa karibu na mwanamuziki na mbunge wa upinzani Ribert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine, amefariki dunia kutokana na majeraha, baada ya kutekwa na kupigwa na watu wasiofahamika, jijini Kampala.

Matangazo ya kibiashara

Ziggy Wine alitekwa wiki iliyopita na alipatikana Jijini Kampala siku tatu baadae (Jumamosi ya wiki iliyopita) akiwa ameng’olewa kucha na jicho moja.

Ziggy Wine alikuwa ni mmoja wasanii waliochini ya mwavuli wa People’s Power unaoongozwa na Bobi Wine.

''Jana usiku ndugu yangu, rafiki na msanii mwenza Ziggy Wine alifariki katika hospitali ya Mulago'', Bobi Wine alichapisha katika ukurasa wake wa akaunti ya Twitter.

Sababu za kutekwa msanii huyo bado hazijajulikana na jeshi la polisi nchini humo limeahidi kuwatafuta watekaji hao kwa udi na uvumba.

Kufuatia tukio hilo, Wasanii kibao akiwemo Jose Chameleone wameomboleza msiba huo na kuahidi kutafuta suluhu ya kukomesha vitendo hivyo vya utekaji.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.