Pata taarifa kuu
TANZANIA-MAREKANI-UINGEREZA

Marekani, Uingereza zaeleza wasiwasi kuhusu kuzorota kwa haki za kiraia nchini Tanzania

John Pombe Joseph Magufuli (kushoto) akiapishwa rasmi kuwa Rais wa Tanzania Novemba 5, 2015.
John Pombe Joseph Magufuli (kushoto) akiapishwa rasmi kuwa Rais wa Tanzania Novemba 5, 2015. REUTERS/Emmanuel Herman
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Balozi za Uingereza na Marekani nchini Tanzania zimetoa tamko la kueleza kusikitishwa na kuongezeka kwa uzorotaji wa mchakato wa haki za raia kisheria nchini Tanzania.

Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa hiyo ya pamoja iliyotolewa leo Agosti 9 mwaka 2019 inasema kujidhihirisha kwa matukio zaidi ya mara kwa mara ya watu kutiwa kizuizini kwa muda bila kupelekwa mahakamani na kubadilishiwa mashtaka na mamlaka za kisheria.

Balozi hizo zimesema zinasikitishwa na tukio la hivi karibuni la kushikiliwa kwa mwanahabari Erick Kabendera.

"Tuna wasiwasi hasa kwa tukio la hivi karibuni la kukamatwa na kuwekwa kizuizini ikizingatiwa ukweli kwamba alinyimwa haki ya kuwa na wanasheria kwenye hatua za awali za kutiwa kizuizini kwake ambapo ni kinyume na sheria ya makosa ya jinai," zimesema balozi hizo katika taarifa yao ya pamoja.

Balozi hizo zimesema kwa pamoja kuwa zinaisihi serikali ya Tanzania kutoa hakikisho la mchakato wa kutenda haki kisheria kwa raia wake.

Mwanahabari Erick Kabendera anashikiliwa na vyombo vya usalama ambapo awali polisi walisema kwa kushirikiana na idara ya uhamiaji wanamhoji kuhusu uraia wake kabla ya tena kufunguliwa mashtaka ya ukwepaji wakodi na utakatishaji wa fedha.

Wanaharakati ndani na nje ya Tanzania wamekuwa wakipaza sauti kushinikiza kuachiliwa huru kwa mwanahabari huyo ambaye amekuwa akiandikia magazeti mbalimbali ya ndani na nje ya Tanzania.

Taarifa ya pamoja ya ubalozi wa Uingereza na Marekani nchini Tanzania
Taarifa ya pamoja ya ubalozi wa Uingereza na Marekani nchini Tanzania https://tz.usembassy.gov/
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.