Pata taarifa kuu
RWANDA-UFARANSA-USHIRIKIANO

Ufaransa/Rwanda: Mchakato wa kuboresha uhusiano kati ya Paris na Kigali waendelea

Ufaransa ina mwakilishi Rwanda, lakini haina balozi.
Ufaransa ina mwakilishi Rwanda, lakini haina balozi. © JOSE CENDON / AFP
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Afisa mpya anayehusika na masuala ya mambo ya kigeni kutoka Ufaransa, ambaye uteuzi wake una mtazamo wa kisiasa, yuko mjini Kigali, nchini Rwanda tangu mwezi Julai, wakati mradi wa kuzindua kituo cha kitamaduni cha lugha ya Kifaransa unatarajiwa kuanza.

Matangazo ya kibiashara

Mnamo Julai 10, Jérémie Blin alichukuwa nafasi ya Etienne de Souza kama afisa anayehusika na mambo ya kigeni kwenye ubalozi wa Ufaransa mjini Kigali.

Wengi waliona kwamba hatua hiyo ni ya kiufundi, na uteuzi huo una mtazamo wa kisiasa. Afisa huyo wa mambo ya kigeni wakati huo alikuwa anashikilia nafasi ya Naibu Mkurugenzi Mkuu wa masuala ya Afrika ya Kati kwenye wizara ya mambo ya kigeni ya Ufaransa (Quai d'Orsay).

Uteuzi wake unaonyesha wazi nia ya Ufaransa ya kuharakisha mchakato wa kuboresha uhusiano na Rwanda.

Hata hivyo Jérémie Blin atakuwa na msaidizi wake katika wiki zijazo, ambaye atachukuwa nafasi "kama ya balozi", chanzo kutoka wizara ya mambo ya kigeni ya Ufaransa kimesema.

Mnamo mwezi Oktoba mwaka jana, Rais wa Rwanda Paul Kagame, akizungumza na RFI na France 24, alisema anatumai kuwa uhusiano wa nchi yake na Ufaransa utaendelea kuimarika.

Matamshi ya Rais Kagame yalikuja baada ya kuchaguliwa kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi yake Bi. Louse Mushikiwabo kuwa Katibu Mkuu mpya wa Umoja wa nchi zinazongumza lugha ya Kifaransa, La Francophonie, na kuungwa mkono na Ufaransa.

Uhusiano wa mataifa hayo mawili, uliingiliwa na dosari baada ya mauaji ya kimbari mnamo mwaka 1994 ,wakati Rwanda ilipoitumu Ufaransa kuhusika katika mauaji hayo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.