KENYA-SOMALIA-BAHARI-SIASA-BAHARI

Rais Kenyatta na Farmajo wakubaliana kurejesha uhusiano wa nchi zao

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta (Kushoto), rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi  na rais wa Somalia  Mohamed Abdullahi Farmaajo wakiwa jijini New York on September 24, 2019.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta (Kushoto), rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi na rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Farmaajo wakiwa jijini New York on September 24, 2019. PHOTO | COURTESY | VILLA SOMALIA 

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na mwenzake wa Somalia Mohamed Farmaajo wamekubaliana kurejesha ushirikiano kati ya nchi zao, lakini wameshindwa kukubaliana kuhusu mzozo wa mmiliki wa eneo la Bahari Hindi.

Matangazo ya kibiashara

Wawili hao wamekutana ana kwa ana na kwa mara ya kwanza baada ya kufanya hivyo mwezi Machi.

Viongozi hao walikutana jijini New York pembezoni mwa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa unaoendelea nchini Marekani.

Mkutano huo uliongozwa na rais wa Misri Abdelfattah al-Sisi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, ikiwa ni hatua ya kwanza ya kuimarisha uhusiano kati ya Nairobi na Mogadishu.

Kenya imeendelea kusisitiza kuwa inataka mzozo wa mmiliki wa eneo la Bahari lenye utajiri wa mafuta na gesi, kutatuliwa kwa njia ya mazungumzo na imekuwa ikishinikiza serikali ya Somalia ikitaka kesi hiyo kutatuliwa Mahakamani.

Kesi hiyo inatarajiwa kuanza mwezi Novemba.