SUDANI KUSINI-USALAMA-SIASA

Sudani Kusini: Wasiwasi watanda kabla ya kurudi kwa Riek Machar Sudani Kusini

Kiongozi wa waasi wa Sudani Kusini Riek Machar wakati wa kutia saini mkataba wa amani na serikali ya Sudani Kusini mwaka 2018.
Kiongozi wa waasi wa Sudani Kusini Riek Machar wakati wa kutia saini mkataba wa amani na serikali ya Sudani Kusini mwaka 2018. © REUTERS

Mvutano unaendelea kuongezeka nchini Sudani Kusini wakati tarehe ya mwisho ya Novemba 12 inakaribia. Siku hiyo, kiongozi wa waasi Riek Machar anatarajiwa kurudi Juba kushikilia nafasi ya makamu wa kwanza wa rais, kabla ya serikali ya umoja wa kitaifa kuundwa.

Matangazo ya kibiashara

Mara ya mwisho Riek Machar kurudi nyumbani ilikuwa mwaka 2016. Lakini vita vilianza tena mara baada kurudi nchini Sudani Kusini. Alitarajiwa kurudi nchini Sudani mnamo mwezi Mei. Lakini muda wa Miezi sita uliongezwa ili aweze kujianda kurudi. Hata hivyo inaonekana kuwa mambo hayajawa tayarikwa Riek Machar kuweza kurudi nchini Sudani Kusini.

Zaidi ya mwaka mmoja baada ya kutiwa saini mkataba wa amani, utekelezaji wake umechelewa sana. Wadadisi wanasema bado kuna kuna masuala mawili ambayo ni muhimu: usalama ili kiongozi wa waasi Riek Machar aweze kurudi nchini na kugawan amadaraka katika ngazi mbalimbali za nchi. Rais Kiir anashutumiwa kutaka kuweka mbele kabila lake la Dinka kwenye nyadhifa mbalimbali za uongozi wa nchi.

Utawala kwa upande wake, unasema unahitaji msaada wa kifedha wa kimataifa ili mambo yaweze kwenda haraka. Ofisi ya rais ilikuwa imeomba dola milioni 100. Zaidi ya dola milioni 10 zilitolewa.

Wakati huo huo Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini David Shearer, ameonya kuwa iwapo viongozi wa nchi hiyo hawatatoa kipaumbele kwa uundwaji wa serikali ya pamoja mwezi ujao, basi mkataba wa amani uliotiwa saini mwaka uliopita utavunjika.